Mauricio Pochettino atajwa PSG, Dele Alli ni kipaumbele chake

Mauricio Pochettino anatarajiwa kumfanya kiungo Dele Alli wa Tottenham Hotspur kuwa miongoni mwa safu yake katika kikosi cha Paris Saint-Germain (PSG), anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mauricio Pochettino yupo tayari kwa kazi. (Picha na Chris Brunskill/Fantasista/Getty Images/ Diramakini ).

Magazeti mengi nchini Ufaransa yanadokeza kuwa, kocha huyo wa zamani wa Spurs amepiga hatua kubwa katika mazungumzo yatakayomshuhudia akiingia kandarasi na PSG baada ya kumtimua Thomas Tuchel. 

Kocha Pochettino ambaye ni raia wa Argentina, hajawahi kupata kikosi cha kumwajiri tangu atimuliwe na Spurs zaidi ya miezi 10 iliyopita kwa sasa. 

Licha ya kuonekana wazi kuwa anapatamani Manchester United, kocha Pochettino anatajwa kuwa, yupo tayari kuinoa PSG huku akiwa ameshaweka mipango kabambe ya kukifanya kikosi hicho kuwa tishio.

Gazeti la L’Equipe linadai kuwa, kocha Pochettino anatarajiwa kutambulishwa rasmi kwa mashabiki na wachezaji wa PSG wiki ijayo katika hatua itakayomshuhudia akirejea kukinoa kikosi hicho alichowahi kukichezea kati ya 2001 na 2003 ikiwa ni miaka mingi iliyopita.

Post a Comment

0 Comments