Mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere afariki

Januari Mosi, 2021 familia ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere imepata msiba wa mtoto wao, Rosemary Nyerere aliyefariki jioni jijini Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Rosemary Nyerere enzi za uhai wake.
Wanafamilia akiwemo Sophia Nyerere na Manyerere Jacton wamethibitisha kifo cha Rosemary Nyerere huku Sophia Nyerere akiandika katika mtandao wa Instagram kuwa shangazi yake amefariki.  

Taarifa zaidi kuhusu msiba zitatolewa hapo baadaye na Familia ya Marehemu. Rosemary ni miongoni mwa watoto saba wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Post a Comment

0 Comments