Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuwahutubia Watanzania leo

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe.Freeman Mbowe leo Januari 3, 2021 anatarajia kuzungumza na Watanzania, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe.Freeman Mbowe (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Mhe. John Mnyika. (Picha na Maktaba).

Mmoja wa maafisa waandamizi kutoka CHADEMA, amemdokeza Mwandishi Diramakini kuwa, Mheshimiwa Mbowe anatarajia kuwahutubia Watanzania kuanzia saa 1:00 jioni ya leo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Kwa mujibu wa afisa huyo, ambaye hakupenda kueleza kwa kina kuhusiana na hotuba hiyo amebainisha kuwa, hotuba ni muhimu kwa Watanzania wote.

"Msubiri Mheshimiwa Mbowe atasema alichokusudia kukisema kwa Watanzania mwenyewe, mimi sina mengi ya kuwaeleza, nikutakiea kazi njema ya uhabarishaji,"ameeleza Afisa huyo kutoka ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Hotuba ya leo Januari 3, 2021 inatarajiwa kuwa ya kwanza ndani ya mwaka huu kutoka kwa Mheshimiwa Freeman Mbowe ambaye amekuwa kimya kwa muda sasa.

Post a Comment

0 Comments