Omar Rekik asajiliwa Arsenal

Klabu ya Arsenal imethibitisha kumsajili, Omar Rekik (19) kutoka katika klabu ya Hertha Berlin ya Ujerumani, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Omar Rekik ambaye ana umri wa miaka 19 amesajiliwa kutoka Hertha Berlin. (Picha na Arsenal/ Diramakini).

Rekik anatajwa kuwa mtu wa kwanza kupewa kanadarasi katika klabu hiyo kwa mwaka huu ambapo uhamisho wake umegharimu Euro milioni 55 (zaidi ya sh.milioni 150).

Klabu hiyo ya Arsenal waliazimia tangu awali kuingia kandarasi na kinda huyo tangu mwanzoni mwa msimu huu, lakini ikashindikana kutokana na taratibu za usajili katika Ligi ya Uingereza na Ujerumani tangu Oktoba 5, 2020.

Awali taarifa kutoka katika klabu hiyo imebainisha kuwa,Rekik ametia saini mkataba wa kitaaluma na Arsenal na atatarajiwa kuchezea mwanzo kikosi cha chipukizi wasiozidi umri wa miaka 23 kabla ya kuanza kupangwa katika kikosi cha kwanza cha watu wazima.

Mzaliwa huyo wa Uholanzi amewahi kuchezea timu ya chipukizi nchini Tunisia na Uholanzi pia amewahi kuvalia jezi za Feyenoord, Manchester City, PSV Eindhoven na Olympique Marseille.

Post a Comment

0 Comments