Papa Francis afanya marekebisho sheria ya Kanisa Katoliki, wanawake kuchukua majukumu

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amefanya marekebisho rasmi ya sheria ya kanisa hilo ili kuruhusu wanawake kuchukua majukumu zaidi kinyume na ilivyokuwa hapo awali, anaripoti Mwandishi Diramakini (Mashirika).
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis. (Picha na Vatican/ Diramakini).

Sheria hiyo mpya kwa jina la Roho ya Mungu (Kiilatino inatajwa Spiritus Domini) inaruhusu wanawake kuhudumu kanisani kwa kusaidia makasisi. 

Aidha, hatua hiyo inaendana na ahadi aliyotoa awali ya kufanya marekebisho kwenye Kanisa Katoliki ambalo kihistoria limekuwa likihudumiwa na wanaume. 

Sheria hiyo inatajwa kuwa itaimarisha zaidi msingi wa kanisa pamoja na kuhusisha kila mmoja kwenye shughuli za uinjilisti ingawa Papa Francis amesema kuwa jukumu la kuhubiri bado litabaki kwa wanaume. 

Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria za kanisa hilo, wanawake hawawezi kuwa makasisi ingawa mwaka 2020, Papa Francis alibuni tume ya kuchunguza iwapo wanawake wapewe nafasi ya kuhudumu kama makasisi katika siku za usoni.

Kutokana na hatua hiyo, wanawake watapewa nafasi ya kuhubiri na kubatiza, lakini si kuongoza misa. Wakati huo huo, hatua hiyo inatajwa kuwa moja wapo ya mafanikio makubwa katika Kanisa kwa kuwa, wanawake nao wana uwezo sawa wa kuwaongoza watu katika kumtumikia Mungu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news