Pep Guardiola ana mpango wa kustaafu

Pep Guardiola (49) ambaye ni kocha wa Manchester City amesema huenda akaendelea katika nafasi ya kuendelea kuwanoa wachezaji kwa muda mrefu tofauti na matarajio yake, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Pep Guardiola amesema ana mpango wa kustaafu kwa sasa. (Picha na AFP/ Diramakini). 

Kocha huyo ameyabainisha hayo ikiwa siku za nyuma amewahi kubainisha kuwa, atastaafu katika soka mapema ili kwenda kufanya mambo mengine. Mapema mwaka huu atatimiza umri wa miaka 50.

“Nilidhani, awal ningejiondoa katika ulingo wa soka mapema kama nilivyokuwa nimepanga. Sasa sioni uwezekano wa hayo kutimia na huenda nikalazimika kusukuma gurudumu hili la mafunzo hadi uzeeni. Hivyo, sijui itakuwaje,”amekaririwa Guardiola.

Kocha huyo wa zamani wa Bayern Munich (miaka mitatu) na Barcelona (miaka minne) ambaye ni raia wa Hispania huku akielekea katika umri wa uzee Novemba, mwaka jana aliingia kandarasi mpya Manchester City ambao amewashindia mataji sita tangu msimu wa 2016-17.nchini Ujerumani kwa miaka mitatu.

Post a Comment

0 Comments