Rais Dkt. Mwinyi afanya mabadiliko uteuzi wakuu wa wilaya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya mabadiliko kwenye uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika Desemba 28, 2020, anaripoti Mwandishi Maalum Diramakini.
Walioteuliwa ni Rashid Simai Msaraka ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Suzan Peter Kunambi anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A”, Hamida Mussa Khamis anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B”, Sadifa Juma Khamis anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A”, Aboud Hassan Mwinyi anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B”. 

Wengine ni Rashid Makame Shamsi anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Marina Joel Thomas anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati, Mgeni Khatib Yahya anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete, CDR Mohammed Mussa Seif ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Abdallah Rashid Ali anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake na Issa Juma Ali ambaye bado uteuzi wake unaendelea katika Wilaya ya Mkoani. 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zanzibar, Hassan Khatib Hassan wakuu hao wapya wa wilaya wataapishwa siku ya Jumaatatu ya Januari 4, 2021 saa 10 jioni.

Post a Comment

0 Comments