Rais Dkt. Mwinyi afungua Skuli ya Sekondari Hasnuu Makame Kibuteni

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea majengo ya Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kuifungua skuli hiyo ikiwa ni shamrashamra za Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar huku akimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said, kulia kwa Rais na kushoto kwa Rais ni Mkurugenzi wa Idara ya Sekondari, Bi. Asia Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Mhandisi Dkt. Idrisa Muslim Hija.(Picha na Ikulu/Diramakini).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kuifungua Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe Rashid Hadidi Rashid na kulia kwa Rais ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwalimu wa Somo la Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja na kulia kwa Rais ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na kushoto kwa Rai ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe.Simai Mohammed Said na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Idrisa Muslim Hija wakati akitembelea Maabara ya Skuli hiyo baada ya kuifungua leo ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame Kibuteni Mkoa wa Kusinin Unguja ikiwa ni shamrashamra za Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu).   

No comments

Powered by Blogger.