Serikali yakipongeza Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake nchini

Serikali imefurahishwa kwa kazi zinazofanywa na Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) katika kupigania haki nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika Januari 7, 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu Tanzania (BoT) jijini Mwanza. 

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba ameyasema hayo wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika jijini Mwanza.

Amewataka majaji hao kuendelea kuongeza na kuimarisha Haki za Wanawake katika suala la Haki Sawa kwa Wote, kukuza upatikanaji wa haki kwa wanawake, kukuza na kuendeleza uongozi wa Mahakama.

Pia kufanya tafiti za kisheria katika Usawa wa Kijinsia na Haki za Binadamu, kubadilishana taarifa katika masuala tata yanayowahusu wanawake na kuondoa upendeleo wa kijinsia na ubaguzi wa aina yeyote.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba akikabidhiwa Tuzo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake (TAWJA), Jaji Joaquuine De-Mello kwa kutambua mchango wake kwa majaji na mahakimu wanawake mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) jijini Mwanza.
Jaji Mkuu wa Tanzania,Prof. Ibrahim Hamis Juma akikabidhiwa Tuzo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake (TAWJA), Jaji Joaquuine De-Mello ya kutambua mchango wake kwa Majaji na Mahakimu wananwake wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) jijini Mwanza.

Amesema kuwa, mtazamo mkubwa wa TAWJA ni kuhakikisha majaji wanawake na mahakimu pamoja na maofisa wengine wa Mahakama na Washirika wanaandaliwa kwa kuwapatia nyenzo sahihi na muhimu zinazohitajika katika kukuza Haki Sawa kwa Wote (‘Equal Justice for All’)

“Ninafahamu kuwa mmekuwa mkifanya hivyo bila kuchoka kwa kipindi cha miaka ishirini (20) mfululizo tangu TAWJA kuanzishwa kwake mwaka 2000,"amesema. 
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda akisisitiza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika jijini Mwanza.

"Kwa hili niwapongeze sana Wanachama wote, mnatakiwa kujivunia na kutembea kifua mbele kwa kazi nzuri mnazofanya. Naamini kuwa hili lisingewezekana bila msaada mkubwa kutoka kwa Mahakama ya Tanzania Bara na Zanzibar,”amesema Dkt.Mwigulu

Dkt.Mwigulu amesema ni wazi kuwa sauti zao Majaji na Mahakimu Wanawake ikijumuisha na zile za wadau wengine nchini zimepelekea utayari, uwazi na hamasa katika kulaani ubaguzi na ukiukwaji wa Haki za Binadamu unaofanywa na wanajamii katika maeneo yetu.
Jaji Mkuu wa Tanzania,Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA), Jaji Joaquline De-Mello akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika jijini Mwanza.

Waziri Dkt. Mwigulu amesema kuwa kaulimbiu ya Mkutano huo ni; “Weledi na Ustawi wa Majaji na Mahakimu Wanawake: Chachu ya Mabadiliko”, imekuja wakati muafaka na mahali sahihi kwani mara nyingi wanawake wataalamu hawatilii maanani ustawi wao na hasa maofisa wa Mahakama ambao muda wote hutingwa zaidi na majukumu yao ya msingi.

"Kutokana na kaulimbiu hiyo, mtaibua vitu vingine vilivyojificha na vinayowakabili maofisa wa mahakama.Maendeleo ya mwanamke ni maendeleo ya wote. Hivyo ni lazima kumpa mwanamke kipaumbele. Ni muhimu sana kumpa mwanamke nafasi nyingi bila kujali kuwa ni haki yake ya msingi kwani pia ni kuonesha matumizi mazuri ya uelewa wa uchumi,"amesisitiza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news