Shilatu aagiza viongozi wa bodi ya Ngonda Amcos wakamatwe

Afisa Tarafa ya Mihambwe iliyopo Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, Emmanuel Shilatu ameagiza kukamatwa kwa uongozi wa bodi nzima ya Chama cha Msingi cha Ngonda kufuatia upotevu wa magunia 10 ya wakulima, anaripoti Mwandishi Diramakini (Mihambwe).

Gavana Shilatu ametoa maelekezo hayo leo Januari 18, 2021 kufuatia lalamiko lililoletwa kwake na Bi. Fadina Hassan aliyefika kulalamika juu ya kutokulipwa kilo 100 alizopima ghalani tangu Oktoba 23, 2020 ambapo Mwenyekiti wa Ngonda Amcos, Rashid Lingoni alikiri kutambua deni hilo mara baada ya kubanwa na Gavana Shilatu juu ya upotevu huo.
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu akizungumza na Mkulima, Bi. Fadina Hassan pamoja na Mwenyekiti Ngonda Amcos Rashid Lingoni ofisini kwa Afisa Tarafa (hawapo pichani) wakati akitoa maelekezo ya kukamatwa kwao. 

“Sijaridhishwa na maelezo ya Mwenyekiti yamejaa ubabaishaji mwingi na kazi yetu Serikali ni kutatua kero za wananchi wakiwemo wakulima ambao wanafanya kazi zao na hatutakubali jasho lao lichezewe. Hivyo nimetoa maelekezo viongozi hao wa Amcos wakamatwe mara moja,”amesema Gavana Shilatu wakati akizungumzia tukio hilo. 
Mkulima Bi. Fadina Hassan pamoja na Mwenyekiti Ngonda Amcos, Rashid Lingoni wakiwa Kituo cha Polisi cha wilayani Tandahimba kufuatia agizo la Afisa Tarafa Mihambwe, Emmanuel Shilatu aliyeagiza kukamatwa kwa uongozi wa bodi nzima ya Ngonda Amcos. 

Gavana Shilatu amewataka viongozi wa Amcos wenye michezo hiyo michafu waache mara moja na wahakikishe wamewalipa wakulima fedha zao.

Pia amewasihi wananchi kuendelea kufanya kazi ipasavyo na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wapo tayari wakati wote kulinda maslahi yao ili kila tu anufaike na jasho lake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news