Simba SC, Namungo FC kuanza maandalizi ya kibabe michuano ya Kimataifa

Simba SC wamepangwa Kundi A pamoja na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na El Marreikh ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Katika ratiba iliyotolewaleo, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye washambuliaji Watanzania, Thomas Ulimwengu na Eliud Ambokile imepangwa Kundi B na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Hilal ya Sudan na CR Belouizdad ya Algeria.

Nao Wydad Casablanca yenye kiungo mshambuliaji Mtanzania, Simon Msuva imepangwa kundi C na Horoya AC ya Guinea, Petro Atletico ya Angola na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Huku Esperance ya Tunisia imepangwa kundi D na Zamalek ya Misri, MC Algiers ya Algeria na Teungueth ya Senegal.

Simba SC itaanzia ugenini na AS Vita Februari 12,2021 mjini Kinshasa kabla ya kuja kuwakabilia Al Ahly jijini Dar es Salaam Februari 23,2021.

Aidha, watakamilisha mzunguko wa kwanza kwa mchezo mwingine wa ugenini dhidi ya El Merreikh nchini Sudan Machi 5,2021.

Katika raundi ya pili Wekundu hao wa Msimbazi wataanzia nyumbani dhidi ya El Merreikh Machi 16,2021 kabla ya kuwaalika AS Vita Aprili 2,2021 na kwenda kukamilisha mechi zake nchini Misri kwa kuchuana na Al Ahly Aprili 9,2021.

Wakati huo huo, Namungo FC kutoka mkoani mkoani Lindi itachuana na Primeiro de Agosto ya Angola katika mechi mbili za nyumbani na ugenini kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. 

Namungo FC wataanzia ugenini Februari 14, 2021 kabla ya kurejea nyumbani kwa mchezo wa marudiano Februari 21,2021.

Post a Comment

0 Comments