Simba SC yawafungisha virago Mtibwa Sugar kombe la Mapinduzi

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wamewafuata mahasimu wao Wanajangwani, Yanga SC katika nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya leo kutembeza kichapo cha mabao 2-0 kwa Mtibwa Sugar, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mtanage wa leo kati ya Simba SC na Mtibwa Sugar katika Kombe la Mapinduzi. (Picha na SC/ Diramakini).

Mtanange huo uliopigwa katika dimba la Amaan lilopo Unguja jijini Zanzibar umewakutanisha Simba SC na Mtibwa Sugar.

Awali Yanga SC ilitangulia baada ya kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC na kufikisha alama nne huku Simba SC baada ya mtanange wa leo ikisikisha alama sita.

Ushindi wa leo wa Simba SC ulianza kunogeshwa na kiungo Hassan Dilunga kwa bao la kwanza dakika ya 6 kupitia pasi ya Mohamed Hussein.Kabla maumivu hayajapoa ndani ya dakika 37, Miraji Athuman alitundika bao safi kwa kichwa katika nyavu za Mtibwa Sugar kupitia pasi ya mshambuliaji, Chris Mugalu.

Kutokana na matokeo hayo, Mtibwa Sugar ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo la Mapinduzi wameondolewa rasmi.

Post a Comment

0 Comments