TBS yatoa elimu kwa wafanyabiashara mjini Masasi

Mkaguzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kusini,Barnabas Jacob akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa soko la Mkuti katika Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, ikiwa ni hatua ya shirika hilo kutimiza jukumu lake la utoaji elimu kwa umma. 

Wafanyabiashara hao wamesisitizwa kununua na kuuza bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS ili kumlinda mlaji. 
Pia Afisa Uhusiano Mkuu wa TBS amewakumbusha wauzaji wa nguo za mitumba katika soko hilo kuendelea kufuata maagizo ya serikali kwa kutokununua na kuuza nguo za ndani za mitumba, ambazo haziruhusiwi kisheria. 

Kiwango cha nguo za mitumba hakiruhusu uuzwaji wa nguo za ndani za mitumba kama ville sidiria, chupi na nguo za kulalia kwani zinahatarisha usalama wa mtumiaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news