TCRA yaitaka Wasafi TV kusitisha matangazo miezi sita

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imeitaka Wasafi TV kusitisha kurusha matangazo kwa miezi sita kuanzia leo Januari 5, 2021 kutokana kwa kukiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha maudhui ya utupu, anaripoti Mwandishi Diramakini.
TCRA imesema kituo hicho kimekiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha maudhui yaliyomuonesha mwanamuziki Gigy Money akionesha utupu wake akiwa jukwaani.

Wasafi TV ni miongoni mwa bidhaa zinazomilikiwa na Wasafi Media chini ya CEO wake, Diamond Platinum.


Post a Comment

0 Comments