Wanaotuhumiwa kumuua Rais wa zamani Laurent-Désiré Kabila waachiwa huru

Zaidi ya watu 22 waliokuwa wamehukumiwa kifo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baada ya kupatikana na hatia mwaka 2001 ya kumuua aliyekuwa Rais wa nchi hiyo,Laurent Desire Kabila wameachiliwa huru, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Hayati mzee Laurent-Désiré Kabila wakati wa uhai wake.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, wafungwa hao wakiongozwa na Kanali Eddy Kapend aliyekuwa msaidizi wa rais Laurent-Désiré Kabila waliachiliwa huru baada ya kupata msamaha wa Rais Felix Tshisekedi wa nchi hiyo. 

Uamuzi huo wa Januari 8, 2021 zilisababisha jijini la Kinshasa na miji mingine kurindima kwa shangwe baada ya kuachiliwa huru kwa watu hao 22 katika gereza la Makala na kupokelewa na mamia ya jamaa, ndugu na marafiki kutoka kila kona. 

Aidha, raia wengi nchini DRC wamekuwa wakiamini kuwa, watu hao hawakuhusika na kifo cha rais huyo wa zamani badala yake walikuhumiwa kimakosa. 

Hata hivyo, mashirika ya kutetea haki za binadamu yalilaumu namna mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo ilivyoendesha kesi hiyo. 

Rais wa zamani, Joseph Kabila ambaye alichukua madaraka ndani ya siku nane baada ya kuuawa kwa baba yake, mara kadhaa alikataa wito wa kuachiliwa huru kwa wafungwa hao, licha ya wengine 11 kupoteza maisha wakiwa gerezani. 

Miaka 20 (tangu Januari 16,2001) iliyopita Rais Laurent Desire Kabila alipigwa risasi na mmoja wa walinzi wake katika Ikulu ya Rais na kujeruhiwa vibaya. Siku mbili baadaye, serikali ya Kinshasa ilithibitisha kifo cha Rais Laurent Desire Kabila nchini humo. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news