Watanzania wahamasishwa kuendelea kupendana, kutenda mema

Wito umetolewa kwa Watanzania kuendelea kutenda mema na kuhakikisha kuwa wanakuwa wamoja katika kuandaa vijana kwa ajili ya kuwa viongozi bora wa Taifa la baadaye, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mbunge wa Jimbo la Kijini visiwani Zanzibar, Yahya Ali maarufu Maambaless (katikati) akiwa na Makamu wa Chama Cha NCCR Mageuzi Taifa, Bw. Ambar Khamis Haji pamoja na Msemaji Mkuu wa Taasisi ya Twariqa Tanzania, Haruna Hussein katika ziara yao ya kidini mkoani Arusha.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Taifa,Bw.Ambar Khamis Haji amesema kuwa, nyumba za ibada zikitumika vizuri zitaweza kusaidia kuwa na vijana na viongozi waaminifu pindi wanapokuwa vijana.

Amesema kuwa, kila mwananchi anafaa kufuata maadili mema kwa kuwa vitabu vya dini vinasema kila unapotenda mema basi utalipwa mema.

“Tuendeleeee kushirkiana kama viongozi wetu wa Taifa wanavyoendeleza ushirikiano bila kujali mipaka lengo liwe ni maendeleo tu haswa katika nyanja hii ya dini kwa kuwa nyumba kama hizi zinasaidia sana, kuhakikisha vijana wanakuwa katika maadili mema na tunapata viongozi wazuri hivyo tutaendelea kuboresha ushirikiano na umoja huu,”amesema Ambar.

Nae Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Jimbo la Kijini, Yahya Ali Khamis maarufu kama Maambaless amesema kuwa, ziara hiyo mkoani Arusha ni mwaliko wa taasisi ya dini ya kiislamu ya Twariqa Tanzania ambayo lengo ni kushirikiana katika changamoto mbalimbali na kukuza taasisi hiyo.

Bw.Yahya ameahidi kumalizia ujenzi wa jengo la msikiti wa Ngarenaro ambao ni msikiti mama unaotumiwa na taasisi hiyo pamoja na kununua ardhi kwa ajili ya ujenzi wa msikiti na madrasa katika eneo Kata ya Terati.

“Ndugu zangu tuendeleze ushirikiano huu kama ambavyo wanafanya Marais wetu Dkt.John Pombe Magufuli na Dkt.Hussein Mwinyi tuchape kazi bila kujali mipaka mradi tu hatuvunji sheria,penye shida tuitangaze na tusaidiane ili tumalize msikiti huu,”amesema Mbunge huyo.

Kwa upande wake Sheikh Haruna Hussein ambaye ni Msemaji wa Taasisi ya Twariqa Tanzania amesema kuwa, ujio huo una maana kubwa kwa taasisi hiyo na daima wataendelea kudumisha Muungano ambao uliasisiwa na viongozi wa kwanza wa nchi.

Haruna amesema kuwa, nia ya viongozi hao ni kuweza kuhakikisha kuwa wanashirikiana kuleta maendeleo katika Mkoa wa Arusha na kuhakikisha kuwa baadhi ya changamoto zinatatuliwa.

Ziara ya kidini kwa viongozi hao kutoka visiwani Zanzibar ni kuongeza ushirikiano wa kidini ambapo pia mbali na kununua eneo hilo wameahidi kujenga Msikiti na Madrasa na kutatua changamoto nyingine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news