Waziri Jafo afurahishwa na stendi mpya ya Bariadi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Selemani Jafo amefurahishwa na ujenzi wa stendi ya mabasi mjini Bariadi iliyojengwa kupitia mradi wa uboreshaji wa miji unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika baadhi ya Manispaa na halmashauri za miji hapa nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Muonekano wa majengo ya stendi mpya ya kisasa.

Stendi hiyo kubwa ya mabasi ilijengwa sambamba na barabara ya lami ya kilomita 1.5 na imegharimu jumla ya shilingi bilion 7. 

Waziri Jafo amewaagiza viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kutunza miundombinu yote ikiwemo stendi, barabara, mifereji na taa za barabarani ambazo zimeubadilisha Mji wa bBriadi kwa kiasi kikubwa. 
Waziri Jafo akiteta jambo na baadhi ya viongozi waandamizi.

Aidha,Jafo amewataka watendaji wa halmashauri hiyo kusimamia ukusanyaji wa mapato katika stendi hiyo ili kuweza kupata fedha za kujenga miradi ya huduma za jamii. 

Meneja msimamizi wa stendi hiyo ameagizwa kutumia mifumo ya kielekroniki ili kuzuia upotevu wa mapato ya halmashauri hiyo.

Post a Comment

0 Comments