Waziri Mkuu ashiriki maziko ya Rosemary Nyerere

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki maziko ya mtoto wa Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rosemary Nyerere aliyefariki dunia Januari Mosi, 2021, anaripoti Mwandishi Diramakini (Dar es Salaam). 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo katika kaburi la Rosemary Nyerere ambaye ni Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambara Nyerere katika maziko yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo katika Kituo cha Hija Pugu jijini Dar es Salaam leo Januari 6, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Maziko hayo ya Rosemary Nyerere yamefanyika leo Januari 6, 2021 katika makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo kwenye Kituo cha Hija kilichoko Pugu jijini Dar es Salaam. 

Ibada ya mazishi imeongozwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki Upanga jijini Dar es Salaam, Dias Mario. 

Viongozi wengine walioshiriki katika maziko hayo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Mama Sitti, Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba. 

Wengine ni mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa, Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula. 

Viongozi wengine ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi, Spika Mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakary Kunenge na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news