Barcelona yaichapa Elche mabao 3-0 La Liga

Klabu ya Barcelona imeichapa Elche mabao matatu usiku huu wa Februari 24, 2021 katika mchuano wa La Liga, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mtanange dhidi ya Barcelona na Elche katika dimba la Camp Nou. (Enric Fontcuberta - Enric Fontcuberta / EFE)

Ushindi wa Barcelona ulianza kunogeshwa na Lionel Messi ndani ya dakika ya 48 kwa kuzitikisa nyavu za Elche na dakika ya 68 akaweka kambani mkuki mwingine ndani ya dimba la Camp Nou.

Aidha, kabla kidonda akijapoa dhidi ya Elche, Jordi Alba ndani ya dakika 73 akafunga hesabu kwa kuweka kambani goli safi ambalo limeiwezesha Barcelona kujitwalia alama zote tatu kwa ushindi mnono.

Kwa ushindi huo Barcelona imejikusanyia alama 50 ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Real Madrid ambayo ipo nafasi ya pili kwa alama 52 huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Atletico Madrid ambayo imejikusanyia alama 55.

Wakati huo huo,Elche wapo nafasi ya pili mwisho kwa maana ya 19 ikiwa na alama 21 huku anayefunga hesabu katika msimamo huo akiwa mkiani ni Huesca kwa alama 19 akiwa nafasi ya 20.

Post a Comment

0 Comments