Benki ya Exim yaendelea kuunga mkono juhudi za uboreshaji elimu Zanzibar

Benki ya Exim imetoa kiasi cha sh.milioni 10 kwa Taasisi ya Asma Mwinyi Foundation (AMF) kwa ajili ya kuwezesha ununuzi wa vifaa vya ujenzi na ukarabati wa vyoo vya Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Kandwi iliyopo Unguja jijini Zanzibar, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hatua hiyo ni sehemu ya dhamira endelevu ya benki hiyo katika kusaidia sekta za elimu na afya nchini.
Uongozi wa benki hiyo ukikabidhi hundi kwa ajili ya kufanikisha ununuzi wa vifaa.

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Bw. Stanley Kafu, aliwasilisha msaada huo kwa Bi Asma A.H Mwinyi ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi AMF katika hafla ya makabidhiano ambayo ilifanyika katika viwanja vya shule hiyo jijini Zanzibar.

“Tumejitolea kuhudumia watu, biashara na jamii kwa ujumla. Benki ya Exim na AMF kwa pamoja tuna dhamira inayofanana ya kusaidia juhudi za kielimu na ustawi wa wanafunzi wetu na shule kote nchini. Wanafunzi hutumia muda mwingi zaidi katika siku wakiwa shuleni hivyo ni muhimu zaidi tukiweka jitihada katika kuboresha mazingira ya vyoo vyao,” amesema.

“Tunafurahi kuwa sehemu ya mkakati huu muhimu unaolenga kuinua mazingira ya elimu Zanzibar. Tunaona kwamba taasisi ya AMF kuwa mshirika sahihi katika kufanikisha dhamira hiyo. Benki ya Exim tumekuwa wadau wakubwa katika kusaidia sekta ya elimu katika jamii yetu, na tunatarajia kupanua juhudi hizo hapa Zanzibar,"ameongeza.

Ikiwa ni taasisi isiyojiendesha kibiashara yenye makao yake nchini, AMF imejikita zaidi katika kukuza programu ambazo zinaboresha maendeleo ya jamii katika mazingira ya vijijini na mijini, kushughulika haswa na wasichana na wanawake wenye mahitaji ya elimu, afya, na mahitaji mengine ya msingi katika jamii zao.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya AMF, Bi. Asma A.H Mwinyi aliishukuru benki ya Exim huku akibainisha kuwa msaada huo utagusa maisha ya wanafunzi wengi kwa miaka mingi ijayo.

“Wadau wetu muhimu na washirika kama Benki ya Exim ndio nguzo muhimu kwa mafanikio yetu. Tunashukuru kwa msaada huu ambao utasaidia katika kukarabati vyoo vya Shule ya awali, Msingi na Sekondari ya Kandwi,”amebainisha.

Kulingana na taarifa ya wasemaji wa shule hizo, Bw Kheir Juma Pandu na Juma Haji Ame walieleza kuwa, kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa vyoo hivyo kutasaidia kuhudumia wanafunzi zaidi 700 waliopo katika shule hiyo.

“Tunatumahi kuwa ukarabati huu utasaidia watoto kuzingatia kwa zaidia masomo yao,” walieleza.

Zaidi alitoa wito kwa taasisi zingine za kifedha na wadau wanaopenda kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule za umma nchini kujitokeza kwa wingi katika jitihada hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news