Dkt.Bashiru afafanua uhusiano wa CCM na Dodoma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally leo amefafanua kwa undani Uhusiano uliyopo kati ya CCM na Mkoa wa Dodoma ambao ndio Makuu Makuu ya Chama kwa sasa, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Katibu Mkuu ameyasema hayo leo tarehe 5 Februari, 2021 katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Dodoma.

Akijibu swali la Mtangazaji wa shirika hilo kuhusu uhusiano uliyopo, amefafanua kuwa,

"Chama Cha TANU ndicho kilicho amua kupitia Halmashauri Kuu ya Taifa mwaka 1973, kwamba Dodoma iwe Makao Makuu, na wakati huo Rais Wa TANU na Rais wa jamhuri ya Muungano Mwalimu Nyerere aliandaa utaratibu wa kuwauliza wananchi na wengi waliunga mkono".

Aidha, Katibu Mkuu akieleza zaidi, amesema Dodoma kuwa Makao Makuu katika kipindi cha awamu ya tano ya uongozi ni kutokana na uamuzi wa TANU, Chama ambacho kiliungana na ASP kuzaa CCM tarehe na mwezi kama wa leo mwaka 1977, hivyo CCM imetekeleza uwamuzi wake, ambao hata kama umechelewa kutekelezwa lakini chini ya Mwenyekiti wa Sasa na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli uamuzo huo umetekelezwa, na kati ya mafanikio mengi katika kipindi hiki, hili ni kubwa zaidi.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu ameeleza malengo mbalimbali ya uundwaji wa CCM, ikiwa ni pamoja kulinda Heshima na Uhuru wa Tanzania na Afrika, kuwaongoza Watanzania katika kujenga jamii ya haki, kuamini katika usawa wa binadamu na kujenga jamii inayojitegemea katika kutatua changamoto zake.

Ikumbukwe kuwa, tarehe na mwezi kama wa leo miaka 44 iliyopita, vyama vya TANU ya Tanzania bara na ASP ya Tanzania Visiwani (Zanzibar) vilivyoanzishwa mwaka 1954 na mwaka1957, viliungana mwaka 1977 na kuunda Chama kimoja Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news