Giround, Werner waipaisha Chelsea Ligi Kuu England

Olivier Giround ndani ya dakika 31 na Timo Werner ndani ya dakika 39 wameifanya klabu yao ya Chelsea kutamba mbele ya Newcastle United baada ya kuondoka na alama tatu zote, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Dimba la Stamfrod Bridge mambo yalikuwa hivi. (Picha na Gettyimages).

Alama hizo zimepatikana kupitia ushindi wa mabao mawili kwa sufuri katika mtanange huo wa Ligi Kuu nchini England uliochezwa katika Dimba la Stamfrod Bridge Februari 15, 2021.

Timo Werner ambaye ni mshambuliaji wa Kimataifa kutoka nchini Ujerumani, bao hilo limemuwezesha kumaliza ukame wa magoli ndani ya Chelsea baada ya kutumia dakika 1000 kufunga bao lake akihitaji mechi 14 ili kuisaidia timu yake kuondoka na alama tatu muhimu mbele ya Newcastle.

Mshambuliaji huyo mbali na kufunga pia alitangulia kusaidia upatikanaji wa bao la kwanza kwa Chelsea, bao ambalo likiwekwa nyavuni na Oliver Giroud ambaye alichukua nafasi ya Tammy Abraham.

Ushindi huo unaifanya Chelsea kukwea mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini England juu ya West Ham United ambao walishinda mechi yao dhidi ya Sheffield United mapema.

Wa kwanza kuwapa shangwe mashabiki wa West Ham alikuwa ni Declan Rice ndani ya dakika 41, Issa Diop ndani ya dakika 58 na Ryan Fredericks akafunga hesabu ndani ya dakika 90+6, hivyo kutoshana alama na Chelsea ingawa zote zinakaa chini ya bingwa mtetezi Liverpool katika Ligi Kuu hiyo.

Post a Comment

0 Comments