Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo akutana na wafanyakazi


Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Khamis Abdallah Said akimkaribisha katibu mkuu wa wizara hiyo kuongea na wafanyakazi wa sekta ya Michezo na Utamaduni huko katika Ukumbi wa Sanaa Raha leo Mjini Unguja. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab akiwasisitiza wafanyakazi nidhamu,mashirikiano pamoja uwajibikaji katika sehemu zao za kazi huko katika Ukumbi wa Sanaa Raha leo Mjini Unguja. Wafanyakazi wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa umakini Katibu Mkuu Fatma Hamad Rajab ( hayupo pichani) wakati akizungumza nao huko katika Ukumbi wa Sanaa Raha leo Mjini Unguja. Msaidizi Meneja Studio za Filamu Abdallah Ally(Duu) akieleza changamoto wanazokabiliana nazo katika maeneo yao ya kufanyia kazi huko katika Ukumbi wa Sanaa Raha leo Mjini Unguja. (Picha zote na MAELEZO Zanzibar).

No comments

Powered by Blogger.