Koffi Olomide: Tanzania ni kama nyumbani, nitaendelea kuwa nanyi




Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akiteta jambo na mwanamuziki galacha duniani katika muziki wa rhumba, Koffi Olomide (Mzee ya Mboka), walipokutana usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Koffi Olomide alikuwa nchini kutumbuiza chini ya mwaliko wa kampuni ya Prime Time Promotions na Clouds Entertainment.

Dkt.Abbasi ametumia muda huo kumshukuru mkongwe huyo kwa kuitangaza Tanzania mara kwa mara ikiwemo kushirikiana na wanamuziki vijana wa hapa nchini kuinua na kuutangaza muziki wao. 

Koffi ameahidi kuendelea kusaidia kukuza vipaji vya Tanzania akisema: “Dar es Salaam na Tanzania mimi ni kama nyumbani, nitaendelea kuwa nanyi karibu,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news