🔴LIVE:Rais Magufuli akifungua Daraja la Juu Ubungo (Ubungo Interchange) leo Februari 24, 2021



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua Daraja la Juu katika Makutano ya Barabara za Ubungo (Kijazi Interchange) Ubungo jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Februari 2021.

TAZAMA LIVE HAPA CHINI
Hafla ya Ufunguzi wa Daraja la Juu Ubungo ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kamba kuzindua jina la Daraja la Juu la Ubungo Interchange ambapo kwasasa linaitwa Kijazi Interchange mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kuliita Daraja hilo ili kutambua Utumishi uliotukuka wa Marehemu Balozi Mhandisi John William Kijazi katika sherehe zilizofanyika Ubungo jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Februari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuzindua jina la Daraja la Kijazi Interchange Ubungo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea sehemu ya chini ya la Daraja la Kijazi Interchange Ubungo jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale wakati akivuta utepe kufungua Rasmi Daraja la Juu katika Makutano ya Barabara za Morogoro, Sam Nujoma, na Mandela ambapo kwasasa linaitwa Kijazi Interchange leo tarehe 24 Februari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo mara baada ya kufungua Daraja la Juu katika Makutano ya Barabara za Morogoro, Sam Nujoma, na Mandela ambapo kwasasa linaitwa Kijazi Interchange leo tarehe 24 Februari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea eneo la mkutano mara baada ya kufungua Daraja la Juu Kijazi Interchange Ubungo jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Februari 2021.

Daraja la Barabara za Juu Kijazi Interchange kama linavyoonekana pichani mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulifungua leo tarehe 24 Februari 2021. (Picha zote na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news