Maendeleo Bank yazindua Kampeni ya Upendo Wote Kwako

Maendeleo Benki (Maendeleo Bank) leo Februari 4, 2021 imezindua rasmi Kampeni ya Upendo kwa Wote, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Maendeleo Benki uliopo Posta jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Huduma kwa wataja wa Maendeleo Benki, Syvia Chaula (katikati), akionesha maandishi kuashiria uzinduzi rasmi i wa Kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Kampeni ya Upendo wote kwako wa Maendeleo Benki Eliupendo Mziray pamoja na Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Teknohama wa Benki hiyo George Wandwalo. (Picha na Mwandishi Diramakini).

Meneja wa huduma kwa Wateja wa Maendeleo Benki, Sylvia Chaula wakati akizindua rasmi kampeni ya Upendo Wote Kwako itakayoanza leo hadi Februari 13, 2021 amesema inalenga kuhamasisha wateja wote wa benki hiyo kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank.

Chaula ameeleza kuwa, kilele cha kampeni ya Upendo Wote Kwako kitakuwa ni siku ya wapendanao (Valentine’s day) yaani tarehe 14/02/2021 ambapo washindi watatu watakaoshinda watapata zawadi mbalimbali kama vile kompyuta ndogo (laptop), simu janja, saa pamoja na kupata chakula cha usiku na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Benki, Dkt. Ibrahim Mwangalaba pamoja na jopo la wafanyakazi wa benki hiyo katika Hotel ya Holiday Inn iliyopo Posta.

Meneja wa Huduma kwa wataja wa Maendeleo Benki, Syvia Chaula (katikati), akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Kampeni ya Upendo wote kwako wa Maendeleo Benki Eliupendo Mziray pamoja na Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Teknohama wa Benki hiyo George Wandwalo. (Picha na Mwandishi Diramakini).

Amesema, washindi wote watatu watapata nafasi adhimu ya kuwaalika wapendwa wao katika chakula cha usiku, yaani kila mshindi atakuja na +plus one wake katika siku hiyo ambapo pamoja na chakula cha usiku pia kutakuwa na tukio la washindi kupokea zawadi zao kutoka Maendeleo Benki.

"Unajua maneno matupu hayanogeshi shughuli, siku hiyo ya wapendanao sisi kama Maendeleo Benki tunapenda kutumia muda wetu kuwaonyesha wateja wetu kuwa tunawapenda, tunawajali na kuwathamii ndio mana tumechagua siku hiyo kuwaonyesha wateja wetu upendo tulio nao kwao kwa vitendo na sio maneno,"ameongeza Chaula.

Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Teknohama wa Maendeleo Benki George Wandwalo (katikati), akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Kampeni ya Upendo wote kwako wa Maendeleo Benki Eliupendo Mziray pamoja Meneja wa Huduma kwa wataja wa Maendeleo Benki, Syvia Chaula.(Picha na Mwandishi Diramakini).

Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Benki na Tehama,George Wandwalo amesema, Maendeleo Benki imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma na kuja na majawabu mbalimbali yanayoweza kuwakwamua watu kiuchumi na hivyo kutoka kwenye hali moja ya maisha na kwenda kwenye hatua nyingine.

Maendeleo Bank imekuwa ikifanya hivi kwa kuja na huduma mbalimbali kama vile huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo,wafanyakazi, taasisi, vikundi na huduma nyingine nyingi za kibenki.

No comments

Powered by Blogger.