Mafanikio ya mapambano dhidi ya rushwa Tanzania yatambulika Kimataifa

Tanzania imeendelea kung'ara katika anga za Kimataifa kutokana na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli za kupambana na vitendo vya rushwa nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Brigedia Jenerali John Mbungo.

"Tumewaita hapa ili kupitia kwenu, tuendelee kuujulisha umma kwamba, jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Jemedari wetu Mhe. Daktari John Pombe Joseph Magufuli zinaendelea kufanikiwa na kutambulika Kitaifa, Kikanda na hata Kimataifa.

"Januari 28, 2021, Taasisi ya Utafiti ya Kimataifa ijulikanayo kama Transparency International (TI) imetoa taarifa ya hali ya rushwa kwa mwaka 2020 duniani, ambapo Tanzania imeshika nafasi ya 94 kwa kupata alama 38 kati ya nchi 180 duniani zilizofanyiwa utafiti,"amefafanua Brigedia Jenerali Mbungo.

Amesema, matokeo hayo ni kulingana na kiashiria cha Corruption Perception Index (CPI), kilichoanzishwa mwaka 1995 kwa lengo la kupima hali ya rushwa katika nchi mbalimbali duniani.

"Mtakumbuka kwamba mwak 2015 wakati Serikali ay Awamu ya Tano inaingia madarakani, takwimu za Transparency International za kupima hali ya rushwa nchini zilisema kuwa, tanzania tumepata alama 30/100 na kushika nafasi ya 117 kati ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti.

"Hata hivyo, takwimu zilizotolewa na Transparency International, Januari 28, 2021, zinaonesha kuwa, Tanzania imepata alama 38/ 100 na kushika nafasi ya 94 kati ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti. Haya ni mafanikio makubwa, kwani tumepanda kwa alama 8 na tumezipita nchi 23 ndani ya miaka mitano tu,"amefafanua.

Pia amesema, kulingana na taarifa hiyo, Tanzania imeshika nafasi ya pili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikitanguliwa na Rwanda iliyopata alama 54;
Brigedia Jenerali Mbungo amesema, kwenye Jumuiya ua Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yenye nchi wanachama 15, Tanzania imeshika nafasi ya saba ikitanguliwa na Seychelles iliyopata alama 66, Botswana alama 60, Mauritius alama 53, Namibia alama 51, Afrika Kusini alama 44 na Lesotho alama 41.

Aidha,amesema taarifa inaonesha kuwa, nchi ya Denmark na New Zealand zilishika nafasi ya kwanza duniani kwa kupata alama 88 huku Somalia na Sundan Kusini zikishika nafasi ya 180 kwa kupata alama 12 kila moja.

"Takwimu hizi zinaashiria kwamba, Watanzania tunaendelea kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na vitendo vya rushwa na pia ni mwendelezo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya vema kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika na Dunia nzima kwa ujumla,"amesema.

SABABU ZA MAFANIKIO

Brigedia Jenerali Mbungo amesma kuwa, sababu za mafanikio ni nyingi ila mosi ni dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kudhibiti vitendo vya hongo na rushwa, uchepushaji wa fedha za umma pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

Amesema, kutokana na dhamira hiyo ya Mhe.Rais Dkt.Magufuli, Tanzania imefanikiwa katika usimamizi na udhibiti wa maadili kwa watumishi wa umma pamoja na mikakati mbalimbali katika kupambana na watu  wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.




 Aidha, ili kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na Serikali kugharamia miradi ya maendeleo sehemu mbalimbali nchini zinatumika ipasavyo, TAKUKURU ilifuatilia miradi 3,329 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 12.9.

Amesema, miradi 446 kati ya hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 87 iligundulika kuwa na kasoro au kufantiwa ubadhirifu hivyo uchunguzi wake unaendelea.

TAKUKURU pia imekuwa ikitumia njia mbalimbali za uelimishaji zilizolenga kubadilisha mitizamo ya wananchi dhidi ya rushwa na kuongeza uelewa wao wa masuala ya rushwa.

"Wananchi wanaelezwa kuhusu madhara ya rushwa kwao binafsi na kwa jamii kwa ujumla, mafanikio ya Serikali katika kupambana na rushwa ni pamoja na wajibu wao katika kushiriki mapambano dhidi ya rushwa,"amefafanua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news