Manchester City yaichakaza Tottenham Hotspur 3-0

Klabu ya Manchester City imeendeleza wimbi la ushindi mpaka mechi 15 mfululizo na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini England, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Wachezaji wa Man City wakifurahia ushindi wao dhidi ya Tottenham Hostspur. (Picha na Gettyimages).

Ni baada ya kuitandika Tottenham Hotspur goli 3-0 katika dimba la Etihad mchezo uliopigwa Februari 13, 2021.

Ilkay Gundogan ambaye ni kiungo mshambuliaji wa Ujerumani ameendelea kuwa mwiba kwa wapinzani baada ya kufunga goli mbili.

Aidha,kiungo mkabaji Rodri aliweka nyavuni bao moja kwa penati ambayo kocha Jose Mourinho anasema ni tuta la kisasa kwa sababu ya urahisi kwa mujibu wa maelezo yake.

Wao Spurs wameendelea kuwa na mwenendo wa taratibu baada ya kukusanya alama 16 tu kwenye mechi 14 ambazo imecheza mpaka sasa, wamepoteza mechi nne kwenye mechi tano katika mashindano yote na wanabakia nafasi ya nane katika msimamo.

Rodri alikuwa wa kwanza kuweka nyavuni bao hilo ndani ya dakika 23 huku Ilkay Gundogan akipashika nyavuni mabao yake ndani ya dakika 50 na dakika ya 66.

Post a Comment

0 Comments