Mbunge wa Upinzani atakiwa kuwasilisha ushaidi wizi wa kura

Naibu Spika wa Bunge, Dkt.Tulia Ackson amempa siku nane Mbunge wa Viti Maalum, Felista Njau ambaye ni kati ya wabunge 19 waliovuliwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwasilisha kwa Kamati ya Maadili ya Bunge ushahidi aliodai katika uchaguzi Mkuu wa Jimbo la Kawe yalikamatwa maboksi ya kura yaliyosababisha kumpa ushindi Mbunge wa jimbo hilo,Josephat Gwajima, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson.

Ametoa maagizo hayo leo Februari 3, 2021 baada ya Mbunge huyo kukataa kufuata kauli hiyo huku akidai kwamba ushahidi anao na yupo tayari kuuleta.

"Kanuni ya 70 ya kanuni za Bunge inakataza Mbunge kusema uongo bungeni na fasili ya 4, 5 na 6 zinasema mbunge aliyekataa kufuta kauli kuleta ushahidi,"amesema Dkt.Tulia.

Amesema,Mbunge huyo apeleke ushahidi wake kwa Kamati ya Maadili ya Bunge na kisha maamuzi yatatolewa bungeni.

Akichangia katika hoja ya kujadili hotuba ya Rais ya kufungua Bunge la 12, Mheshimiwa Njau amesema uchaguzi Mkuu haukuwa wa haki huku akitolea mfano Jimbo la Kawe namna ambavyo yalikamatwa maboksi hayo ya kura.

Hata hivyo, Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Askofu Josephat Gwajima amesema alipata ushindi halali wa kura zaidi ya laki moja huku mpinzani wake akipata kura 30,000.

Katika hatua nyingine, Dkt.Tulia amewataka wabunge kusoma kanuni na kuzielewa ili wajue nini wanapaswa kukizungumza wawapo ndani ya Bunge.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news