Mkandarasi ujenzi Kinondoni Studio-Mwananyamala amchefua RC Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge ameonesha kuchukizwa na kitendo cha kusuasua kwa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kinondoni Studio kuelekea Mwananyamala yenye urefu wa Km 4.2 jambo linalopelekea usumbufu kwa wananchi hususani wagonjwa wanaokwenda kupata huduma Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kutokana na hilo RC Kunenge amemtaka Mkandarasi anaetekeleza Mradi huo kutoka Kampuni ya CRSG kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili ifikapo July 30 Barabara iwe imekamilika kwa asilimia 100 na amesema ndani ya Mwezi mmoja kuanzia leo atarudi kukagua maendeleo ya Ujenzi.

Aidha RC Kunenge amewaonya TARURA kutokumuongezea muda Mkandarasi huyo ambapo pia amewaelekeza kuwa wakali na kusimamia kikamilifu mradi huo.

Miongoni mwa Mambo yaliyomkwaza zaidi RC Kunenge ni kuona hadi kufikia Sasa muda wa Mradi umefikia asilimia 62 lakini kazi iliyofanyika ni asilimia 16 huku wahusika wakitoa sababu dhaifu.
Kwa upande wake Makamu Mhandisi Mshauri wa Mradi huo kutoka Kampuni ya HP Gauf Wile John amemuahidi Mkuu wa Mkoa kuwa maagizo aliyotoa watayatekeleza kwa Wakati.

Ujenzi wa Barabara ya Kinondoni studio kuelekea Mwananyamala yenye urefu wa kilomita 4.2 inatekelezwa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya CRSG.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news