Mkuu wa Mkoa wa Singida atangaza fursa zaidi za kiuchumi

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka Wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuwekeza kwenye Mkoa wa Singida kwa kuwa Mkoa huo umebarikiwa kuwa na fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo bado hazijatumika kikamilifu, anaripoti John Mapepele (Singida).

Wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakionyesha bidhaa zao

Akifungua Kongamano la Mwongozo wa Uwekezaji kwenye Mkoa wa Singida kabla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo huo, Dkt. Nchimbi amesema Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa michache nchini ambayo endapo fursa zake zikitumika utachangia katika maendeleo ya Mkoa na nchi kwa ujumla

Amezitaja baadhi ya fursa zilizopo kwenye Mkoa wa Singida kuwa ni pamoja na nishati ya mafuta asilia na gesi, madini, kilimo cha alizeti, korosho,utalii, ufugaji wa nyuki na kuku pia uwekezaji
kwenye sekta ya michezo ambapo amesema ni zamu ya Mkoa wa Singida kuchangia kikamilifu kwenye uchumi wa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dtk. RehemaNchimbi katikati akiongoza Kongamano la Fursa za Uwekezaj ikwenye Mkoa wa Singida, Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Sheen, kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi.

Akitoa mada kuhusu Uwekezaji wa Alizeti mkoani Singida,Mratibu wa Utafiti wa Alizeti nchini, Frank Reuben amesema zao la alizeti ndiyo zao pekee linaloweza kuuvusha mkoa wa Singida kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa mkoa wa Singida ndiyo unaongoza hapa nchini kwa kulima zao hilo.

Ametaja baadhi ya maeneo ya fursa za uwekezaji kwenye kilimo cha Alizeti kuwa ni pamoja na uzalishaji na usambazaji wa mbegu, Kilimo bora (mesto) cha alizeti na ufugaji nyuki (Agro-apiculture) na uendelezaji wa viwanda vya kuchakata alizeti, chakula cha mifugo na mazao ya nyuki

Mtafiti wa zao la Korosho, kutoka Taasisi ya Utafiti wa mazao ya Kilimo (TARI) Dkt. Fortunatus Kapinga akitoa mada ya zao la Korosho nchini amesema Mkoa wa Singida una ardhi nzuri
yenye rutuba ambayo inafaa sana kwa zao la korosho ukilinganisha na mikoa mingine hapa nchini hivyo ni fursa pekee kwa wawekezaji kuja kufanya uwekezaji katika mkoa huu.

Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Singida (kwenye mstari wa kwanza) wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoani Singida.

Amezitaja baadhi ya bidhaa zinazopatikana kwenye zao la Korosho kuwa ni pamoja na juisi, jamu,mvinyo, maziwa na siagi ambapo amesema kauli mbiu ya mkoa kwenye uwekezaji kwamba
“ni zamu yetu” ikitafsiriwa kwa vitendo italeta mageuzi makubwa katika mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wanawake wachimbaji Madini Mkoa wa Singida, Martha Kayaga amepongeza Serikali ya awamu ya Tano inayoongizwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa jitihada kubwa inayofanya kuwashilikisha wachimbaji wazawa kwenye sekta ambapo ameiomba Serikali kuangalia namna bora ambayo itawawezesha wajimbaji wadogo wadogo kupata mitaji hususan vifaa ili waweze kuongeza tija katika sekta hiyo.

Pia Bi. Kayaga ameiomba Serikali kuwaangalia wachimbaji wanawake kwa jicho la pekee kwa kuwa wao ni nguzo muhimu kwenye familia na kwamba asilimia 10 inayotengwa kwenye Halmashauri imekuwa ikielekezwa kwenye sekta nyingine ambapo amesisitiza endapo itaelekezwa kwa akina mama wachimbaji wadogowadogo itasaidia kuinua hali za uchumi kuanzia kwenye ngazi ya kaya na Taifa kwa
ujumla.

Afisa Uhamasishaji Uwekezaji Mkuu kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini, Joyce Shundu akiwasilisha mada ya “Mazingira na Fursa za Uwekezaji Nchini” ambapo amepongeza jitihada na mikakati mbalimbali inayofanywa na Mkoa wa Singida.

Kwa upande wake, Afisa Uhamasishaji Uwekezaji Mkuu kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini, Joyce Shundu akiwasilisha mada ya “Mazingira na Fursa za Uwekezaji Nchini” amepongeza jitihada na mikakati mbalimbali inayofanywa na Mkoa wa Singida kwa kwenye uwekezaji na kutoa wito kwa
wawekezaji kuwahi kuwekeza kwenye fursaza kipekee zinazopatikana mkoani hapa.

Awali katika salamu za utambulisho, Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi amewataka Watendaji wote wa Serikali Mkoa wa Singida kuhakikisha wanajituma kufanya kazi
kwa weledi kwenye utoaji huduma bora kwa wawekezaji ili azma ya Serikali ya kutaka uwekezaji wenye tija itimie na maisha bora kwa watanzania ifikiwe.

Dkt. Lutambi amesema Serikali ya Mkoa imeshaandaa mazingira wezeshi kwa wadau na wawekezaji makini kuja kuwekeza kwa kuzingatia sheria na taratibu
za nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news