Murtaza Mangungu ndiye Mwenyekiti mpya Simba SC

Klabu ya Simba imepata Mwenyekiti mpya ambaye anakuwa mrithi wa mikoba ya Sued Mkwabi ambaye alibwaga manyanga mwezi Septemba 2019, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Uchaguzi wa leo ambao umefanywa na Wanachama waliokidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kulipa ada ya uanachama umefanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.

Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba ni Murtaza Mangungu baada ya kupata kura 802 sawa na asilimia 70.35 akimshinda Juma Nkamia aliyepata kura 330 sawa na asilimia 28.95. Jumla ya kura zilizopigwa ni 1140 na kura 8 sawa na asilimia 0.7 zimeharibika.

Mwenyekiti mpya wa Simba SC, Murtaza Mangungu.

No comments

Powered by Blogger.