Mwenyekiti CCM Mara awapa pole wana Simiyu kwa kuondokewa na Mwenyekiti wao mkoa

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye (No.3) amewapa pole wanachama wa chama hicho Mkoa wa Simiyu kwa kuondokewa na Mwenyekiti wao, Enock Yakobo ambaye amesema alikuwa miongoni mwa viongozi hodari na wachapa kazi, anaripoti Mwandishi Diramakini (Mara).

Yakobo amefariki leo Februari 23, 2021 asubuhi nyumbani kwake Mwanuzi wilayani Meatu hayo yakiwa ni kwa mujibu wa taarifa ya kifo chake zilizotolewa na Katibu Mwenezi wa chama hicho mkoani humo, Mayunga George.

“CCM mkoa wa Simiyu tunasikitika kutangaza kifo cha mwenyekiti wetu wa mkoa, Enock Yakobo kilichotokea leo. Taratibu za mazishi zitatolewa baadaye baada ya kukaa na familia,”ameeleza George katika taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye (No.3).

Kwa upande wake, Kiboye ameeleza kuwa, taarifa za kifo hicho zimemshutua kwani, si kwamba tu kwamba wanachama wa chama hicho mkoani humo wamempoteza mwenyekiti wao, bali wamepoteza Mzee mwenye hekima na ukarimu kwa watu wote.

"Hakika, chama kimepoteza mtu muhimu sana, nichukue nafasi hii kwa niaba ya wana CCM wote mkoani Mara kuwapa pole wana Simiyu kwa kuondokewa na Mwenyekiti wao, Mzee Enock Yakobo wakati wa uhai wake alikuwa mtu mkarimu na mwenye upendo, alikuwa mstari wa mbele kutoa ushauri na maarifa kwa wengine.

"Mimi alikuwa mlezi wangu, amenifundisha mambo mengi ikiwemo kuwa mstari wa mbele kukipigania chama ili kuhakikisha kinastawi na kuhakikisha tunasimamia kikamilifu utekelezaji wa Illani ya Uchaguzi, hivyo tumempoteza mtu muhimu, nichukue nafasi hii kuwapa pole, ndugu, jamaa na marafiki. Ni maombi yangu kwa Mungu amlaze mahali pema. Amen,"amefafanua Kiboye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news