Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi atoa rai kwa jamii kuwathamini watoto yatima

Jamii imetakiwa kuwathamini na kuwajali watoto waliopoteza wazazi wao na wanaoishi katika mazingira magumu ili na wao waweze kupata mahitaji yao ya msingi ikiwemo elimu, makazi na malazi kama wanavyopata wengine, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Uzini, Khamis Hamza Chilo ameyasema hayo leo huko Skuli ya Kidimni wakati wa kutoa msaada wa nguo kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu waliopo ndani ya Jimbo la Uzini uliofadhiliwa na Taasisi ya Noah Development Services Assocition kutoka nchini China.

Amesema, lengo la msaada huo ni kuona watoto hao wanaishi katika mazingira bora na kuvaa vizuri ili wasijiskie tofauti kati yao na watoto wengine katika jamii, hivyo amewaomba wafadhili kutoa misaada ya hali na mali kila hali itapokaporuhusu. 

"Niwaombe ndugu zangu mliotupa tupa msaada huu msichoke kuendelea kutupatia misaada mengine muhimu kila hali zenu zitavyoruhusu na tunawakaribisha taasisi nyengine kuja kutusaidia ili hawa watoto wetu wapate furaha katika utafutaji wao wa elimu,"amesema Naibu Waziri huyo.

Nae Mwakilishi wa jimbo hilo, Haji Shaaban Waziri ameishukuru taasisi hiyo kwa msaada huo walioutoa na kuahidi kuwa msaada huo utatumika na kuwafikia walengwa wailokusudiwa ikiwa ni pamoja na watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu wanaoishi katika Jimbo hilo.

Aidha, amewataka wazee waliokabidhiwa nguo hizo kwa niaba ya watoto hao kuhakisha nguo hizo wanawapatia walengwa waliokusudiwa pamoja na kuzitunza ili ziweze kutumika kwa muda mrefu.

Kwa upande wa Mkurungenzi wa taasisi ya Noah Development Services Association, Bi. Kwan il Park ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaruhusu na kushirikiana nao katika miradi ya kimaendeleo ikiwemo skuli, vituo vya afya na huduma za maji safi na salama kwa vitongoji na vijiji vilivyomo mkoawa Kusini.

Msaada huo wa nguo uliotolewa na taasisi hiyo una thamani ya shilingi million saba na umetolewa kwa watoto 150 ambao miongoni mwao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wa Jimbo la Uzini jijini Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news