Neil Lennon ang'atuka Celtic ikiwa nyuma ya Rangers kwa alama 18

Kocha wa Celtic, Neil Lennon mwenye umri wa miaka 49 ameng'atuka kuwa kocha wa kikosi hicho baada ya kujikuta nyuma kwa alama 18 dhidi ya vinara Rangers inayonolewa na kocha Steven Gerrard, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Lennon alichukua mikoba ya kuwa kocha wa Celtic kwa mara ya pili mwezi Februari 2019 baada ya Brendan Rodgers kuachana na klabu hiyo.
Kocha Neil Lennon. (glasgowtimes).

Hata hivyo baada ya mafanikio makubwa kwa kikosi cha Celtic na kushinda mataji 10 mfululizo ya Ligi Kuu nchini humo sasa Rangers ni kama imefuta udhibiti wa klabu hiyo.

Kocha msaidizi John Kennedy atachukua nafasi ya Mwalimu huyo kwa muda huku miongoni mwa makocha wanaotabiriwa kujaza pengo la Lennon kwa mkataba wa kudumu mwishoni mwa msimu huu ni kocha wa timu ya taifa ya Scotland, Steve Clarke na aliyekuwa kocha wa Real Madrid, Liverpool na Chelsea, Rafael Benitez.

Aidha, kufikia sasa, Celtic wanashikilia nafasi ya pili kwa alama 64 japo wana pengo la alama 18 kati yao na Rangers wanaonolewa na kiungo wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard.

Hata hivyo, Lennon anaondoka Celtic baada ya kuhudumu kwa mafanikio akiwa mchezaji na kocha kwa zaidi ya kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Post a Comment

0 Comments