Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa aongeza kasi kuvipa ufahamu vyama namna ya kujaza fomu za marejesho ya gharama za uchaguzi

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa (ARPP), Sisty Nyahoza akiwasilisha mada mbele ya viongozi wa Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP) wakati wa mafunzo ya namna ya kujaza fomu za marejesho ya gharama za uchaguzi katika ukumbi wa Samwel Sitta zilizopo Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.Warsha hiyo imefanyika Februari 27, 2021. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeendesha mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo watendaji wa Vyama hivyo kuelekea utekelezaji wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 inayotaka wagombea kujaza fomu za marejesho na kuziwasilisha kwa msajili.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa (ARPP), Sisty Nyahoza akifafanua jambo mbele ya viongozi wa Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP) wakati wa mafunzo ya namna ya kujaza fomu za marejesho ya gharama za uchaguzi katika ukumbi wa Samwel Sitta zilizopo Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeendesha mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo watendaji wa Vyama hivyo kuelekea utekelezaji wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 inayotaka wagombea kujaza fomu za marejesho na kuziwasilisha kwa msajili.
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP), Rashid Rai akichangia mada wakati wa mafunzo ya namna ya kujaza fomu za Marejesho ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa vilivyoshiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 jijini Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeendesha mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo watendaji wa Vyama hivyo kuelekea utekelezaji wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 inayotaka wagombea kujaza fomu za marejesho na kuziwasilisha kwa msajili.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP) wakifuatilia mafunzo ya namna ya kujaza fomu za Marejesho ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa vilivyoshiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 jijini Dar es Salaam.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa(ARPP), Sisty Nyahoza (aliyekaa kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP) mara baada ya kumaliza mafunzo ya namna ya kujaza fomu za marejesho ya gharama za uchaguzi katika ukumbi wa Samwel Sitta zilizopo Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa AAFP, Rashid Rai na Mwenyekiti wa AAFP, Said Soud.(Picha na ORPP.

Post a Comment

0 Comments