Rais Dkt. Mwinyi: Ndoto yangu kuifanya Zanzibar sehemu ya kutoa tiba za kibingwa imeanza

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kwamba ile ndoto yake ya kuifanya Zanzibar iwe ni sehemu ya kutoa tiba za kibingwa sasa imeanza, anaripoti Mwandishi Diramakini (Zanzibar).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwapongeza Madaktari Bingwa Wazalendo wa Hospital ya Mnazi Mmoja wa Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (hawapo pichani) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha zote na Ikulu).

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati alipowapongeza madaktari wa Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu cha Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar ambao aliwaaita Ikulu Jijini Zanzibar kwa lengo hilo maalum la kuwapongeza.

Pongezi hizo zimekuja mara baada ya kitengo hicho cha wataalamu hao kumfanyia upasuaji mgonjwa Kelesh Belinda raia kutoka nchini Nigeria ambaye hakuwa na imani ya kutibiwa hapa Zanzibar lakini kutokana na uwezo uliopo wa kitengo hicho cha hapa Zanzibar mgonjwa huyo aliweza kutibiwa na hatimae mara baada ya kupona alianza kuipa sifa Zanzibar na kutoa taarifa katika mitandao ya kijamii.

Rais Dk. Shein alisema kuwa kuna haja ya kuwapongeza madaktari hao kwa kuanza kutoa huduma hizo za kibingwa ambazo ni ngumu jambo ambalo wameonesha kwamba inawezekana katika kutekeleza ndoto zake.apo pichani) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Daktari Bingwa wa Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dkt. Said Idrisa Ahmada, walipofika ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kupongezwa kwa kufanikisha uporeshaji ya Raia wa Nigeria Bi.Kelesh Belinda, iliofanywa na Kitengo cha Upasuaji Hospitali ya Kuu ya Mnazi mmoja Jijini Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akifurahia jambo wakati Profesa Jose Piquer Belloch Rais wa Taasisi ya NED ya Nchini Hispania, wakati mazungumzo na kupongezwa kwa Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika Hopitali ya Taifa ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.

Hivyo, Rais Dk. Mwinyi alikipongeza kitengo hicho cha Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa kazi nzuri wanazozifanya ambazo zimepelekea kuwaita Ikulu kutokana na mafanikio waliyoyapata ambayo yameijengea sifa kubwa Zanzibar.

Hivyo, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa kuna haja ya kuwapongeza kutokana na kazi hizo licha ya kutambua kwamba wanafanya kazi hizo katika mazingira magumu kwani nia ya kurekebisha mazingira magumu ipo.

Alisema kwamba kazi inayofanywa na kitengo hicho ni kutoa tiba kwani wagonjwa wengi waliokuwa wakisafirishwa kwenda Dar-es-Salaam ama nje ya nchi hivi sasa wengi wanatibiwa Zanzibar ambayo hayo ni mafanikio makubwa kwani lengo ni kuhakikisha wananchi wanatibiwa hapa ndani na kupunguza gharama pamoja na kujenga uwezo.

Dk. Mwinyi aliongeza kuwa pia, kitengo hicho kinajenga uwezo wa kufundisha madaktari na tayari kitengo hicho kimeshapata ithibati ya kuweza kuwatibu hata wagonjwa kutoka nje ya Zanzibar sambamba na kuwepo vifaa vinavyopelekea kufanya aina kadhaa za upasuaji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwapongeza Madaktari Bingwa wa Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahami Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.(hawapo pichani) mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 24-2-2021.

Alisema kuwa ile ndoto yake ya kuifanya Zanzibar iwe ni sehemu ya Zanzibar kutoa tiba za kibingwa wataalamu hao wameonesha mfano kwa kuanza na tiba za kibingwa ambazo ni ngumu.

Alisema kuwa waataalamu hao wameonesha kwamba hilo linawezekana na tayari katika Hospitali ya Mnazimmoja wameshajenga uwezo wa miundombinu kwa maana ya majengo, vyumba vya upasuaji, vifaa na kuanza kutoa elimu.

Alisema kuwa hayo yote ni mafanikio makubwa ambayo yamepelekea kutekeleza ndoto yake huku akieleza kwa kutoa mifano ya Hospitali ya Jakaya Kikwete Dar-es-Salaam, ana uhakika iwapo huduma za tiba ya hiyo itatolewa, tiba ya moyo pamoja na kansa sehemu kubwa ya watu wanaopelekwa nje watatibiwa hapa hapa Zanzibar.

Hivyo, Rais Dk. Mwinyi alieleza jambo ambalo linataka kufanywa na Serikali ya Awamu ya Nane ni kujenga miundombinu kwa jengo jipya la kisasa ili kutoa mazingira bora ya kufanya kazi hizo ili kuhakikisha wataalamu kutoka sehemu mbali mbali waje kutoa huduma hizo sambamba na kujenga uwezo wa ndani.  Madaktari Bingwa wa Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo ya kupongezwa kwa kufanikisha upasuaji wa Raia wa Nigeria Bi. Kelesh Belinda, uliofanywa katika Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu ikiongozwa na Dkt. Said Idrisa Ahmada.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari Bingwa wa Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar baada ya kumaliza mazungumzo yake na kuwapongeza kwa kazi nzuri, na waliokaa (kulia kwa Rais) Rais wa Taasisi ya NED ya Nchini Hispania Prof.Jose Piquer Belloch, Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar Dkt.Omar Dadi Shajak na Daktari Bingwa wa Upasuaji Ubongo Mishipa ya Fahamu Dkt.Said Idrisa Ahmada na( kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said Dkt.Abdalla Hasnu Makame na Dkt Juma Mambi.(Picha na Ikulu).

Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa nguvu za serikali zinahitajika katika kuhakikisha mazingira yanakuwa mazuri na kuweza kuwaunga mkono wale wanaotoa msaada wao kwa Zanzibar katika huduma hiyo.

“Leo nimefurahi sana na nakupongezeni kwa kazi nzuri mnayofanya ambayo imekuwa na sifa dunia nzima tunasikia watu mpaka wa nje kwa kazi nzuri mnazofanya”,alisema Dk. Mwinyi.

Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kumpongeza Profesa Jose Piquer Belloch kwa juhudia zake anazozichukua na kusema kuwa mbali ya tiba anayoiotoa pia amekwua akiunga mkono kwa kusaidia vifaa.

Alisema kuwa yeye pamoja na Serikali anayoiongzoa itaendelea kumuunga mkono bingwa huyo kutoka Hispania na kumuhakikishia kwamba anapata kibali cha kuishi na kumuwezesha kufanya kazi muda wote hapa Zanzibar na kuitaka Idara ya Uhamiaji kuhakikisha inampa kibali hicho.

Aidha, aliwataka kuendelea kuwahudumia Wazanzibari na kusema kwamba lengo ni kuhakikisha huduma hizo zote zinapatikana hapa Zanzibar hasa ikizingatiwa azma ya Serikali ya kujenga Hospitali ya Kisasa huko Binguni.

Nae Mkuu wa Kitengo cha upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu cha Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar Dk. Said Idrissa Ahmada alisema kuwa Idara hiyo ilianzishwa rasmi Novemba, 2014.
Aliongeza kuwa kabla ya kuanzishwa kitengo hizo Profesa Joe mnamo mwaka 2008 alifanya upasuaji wa kwanza ambapo alimfayia mtoto aliyetokea Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja na kufanikiwa vyema upasuasaji huo licha ya changamoto ya vifaa iliyokuwepo wakati huo na baada ya hapo ndipo harakati hizo zilianza.

Alisema kuwa Idara hiyo tokea kufunguliwa mwaka 2014 hadi hivi sasa imeshafanya kesi zipatazo 1700 za upasuaji ikiwemo upasuaji wa vichwa maji kwa watoto, migongo wazi kwa watoto, uvimbe katika ubongo, ajali za vichwa, uvimbe katika mishipa ya fahamu, huduma za uti wa mgongo na nyinezo.

Aliongeza kuwa hatua hiyo imepelekea kupunguza asilimia zaidi ya 50 kupeleka wagonjwa nje ya nchi ikiwemo India na kupunguza gharama kwa Serikali huku .

Alifahamisha kuwa wito waliopata Ikulu kwa ajili ya kupongezwa unatokana na tiba waliyoifanya ya raia wa Nigeria Kelesh Belinda waliomfania upasuaji ambapo kabla ya kufanyia huduma hiyo hakuwa tayari kutibiwa kwa kudhani kwamba Hospitali hiyo haina uwezo kwani Hospitali ya Clobal ilishindwa na kuamriwa aende Dar-es-Salaam.

Dk. Said alieleza jinsi hatua za upasuaji huo walivyozifanya na kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa na hatimae mgonjwa huyo anaendelea na shughuli zake huko kwao Nigeria.

Mbali na mafanikio hayo, Dk. Said alitumia fursa hiyo kueleza changamoto walizonazo katika kitengo chao huku akitumia fursa hiyo kwa kumpongeza Profesa Joe kwa kusaidia vifaa katika kitengo hicho.
Mapema Profesa Jose Piquer Belloch ambaye pia, ni Rais wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu inayohusiana na upasuaji wa Mishipa ya Fahamu, Uti wa Mgongo na Vichwa, Maji (NED) ambaye ni raia kutoa Hispania alipongeza mashirikiano anayoyapata hapa nchini huku akiahidi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kutoa huduma hizo.

Daktari Bingwa huyo alitoa pongezi zake kwa Rais Dk. Mwinyi kwa kuwajali madaktari hao na kuwaita Ikulu akiwa na lengo la kuwapongeza kwa kazi zao nzuri wanazozifanya katika kuisaidia jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news