Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi ZRB na PBZ

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi mpya wa Kamishna wa Bodi ya Mapato (ZRB), pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa upande wa Bodi ya Mapato (ZRB), alieteuliwa kuwa Kamishna wa Bodi hiyo ni Salum Yussuf Ali, uteuzi ambao umeanza tarehe 10 Februari,2021.

Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi amemteua Muhsin Salim Masoud kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kuanzia tarehe 10 Februari, 2021.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, Kamishna wa Bodi ya Mapato (ZRB) na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) waliotenguliwa watapangiwa kazi nyengine kadri itakavyoamuliwa.

No comments

Powered by Blogger.