Rais Kenyatta ndiye mwenyekiti mpya EAC, Mathuki achukua nafasi ya Balozi Liberate Katibu Mkuu

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta amekabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na mwenyekiti anayeondoka, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Rais wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.

Makabidhiano hayo ya Februari 27, 2021 yalifanyika baada ya mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya hiyo kufanya mkutano kwa njia ya mtandao.

Wakati huo huo, Dkt. Peter Mathuki ambaye ni raia wa Kenya kwa sasa ndiye Katibu Mkuu mpya wa jumuiya hiyo akichukua nafasi ya Balozi Liberate Mfumukeko raia wa Burundi ambaye amekamilisha muhula wake.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki mkutano wa 21 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika leo tarehe 27 Februari, 2021 kwa njia ya mtandao. (Picha zote na Ikulu).

Kabla ya uteuzi huo, Mathuki alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la nchi za Afrika Mashariki.

Kwenye mkutano huo, ambao pia ulihudhuriwa na rais Paul Kagame wa Rwanda na Makamu Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, viongozi wa nchi wanachama walisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na kudumisha amani.

Hata hivyo, mmoja wa majaji wapya wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, Kathurima M’Inoti aliapishwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news