Rais Magufuli amteua Zepharine Nyalugenda Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Zepharine Nyalugenda Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,Ikulu mjini Chamwino leo Februari 1, 2021.

Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Galeba alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma.

Uteuzi wa Mhe. Galeba unaanza leo Februari 1, 2021 na ataapishwa kesho saa 4:00 asubuhi Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

No comments

Powered by Blogger.