RC Kunenge atoa maagizo kwa viongozi wa mitaa Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewataka Viongozi ngazi Mitaa kuhakikisha wanashughulikia ipasavyo kero na changamoto mbalimbali kwenye mitaa yao na kuhakikisha wanatoa taarifa mapema pale wanapobaini jambo lipo juu ya uwezo wao ili liweze kushughulikiwa na ngazi za juu, anaripoti Mwandishi Diramakini.
RC Kunenge amesema hayo wakati wa kikao chake na Watendaji na Wenyeviti wa mitaa jijini humo ambapo amesema ni jambo la fedhea kuona kiongozi wa ngazi ya juu anashughulikia kero ya mtaa wakati wahusika wa ngazi ya mtaa wapo wanapeta. 

Amewaelekeza Watendaji wa Mkoa huo kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ukusanyaji wa Mapato ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya Mapato, kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ambapo ametaka ukusanyaji wa Mapato usiwe wa kero Wala wa kuua Biashara za watu. 

Hata hivyo amewataka Viongozi wa Mitaa kusimamia ipasavyo suala la usafi wa mazingira kwenye mitaa yao ili kuwakinga wananchi na magonjwa ya Mlipuko.  

Pamoja na hayo RC Kunenge amewasisitiza pia Viongozi hao kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa watu wanaohatarisha usalama ikiwemo kufichua nyumba zinazogeuzwa Madanguro, wanaowahifadhi wahamiaji haramu, wanaowatumia walemavu kujinufaisha na wauzaji wa dawa za kulevya. 

Sanjari na hayo amezielekeza Taasisi za umma zilizopo jiji humo kuhakikisha wanashirikiana na Watendaji wa Mitaa kwakuwa hao ndio wapo karibu na wananchi na ndio wanaozijua zaidi kero za mtaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news