Bao pekee la Ferland Mendy ndani ya dakika 86 limetosha kuzamisha jahazi la Klabu ya Atalanta na kuiwezesha Real Madrid kujikusanyia alama 3 katika Michuano ya UEFA Champions League, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ferland Mendy akiwajibika kwa ajili ya waajiri wake. (Picha na Tiziana Fabi/AFP/Getty Images).
Mtanange huo uliopigwa katika dimba la Estadio Alfredo Di Stefano, Atalanta walijikuta wakicheza pungufu baada ya mchezaji wao Remo Freuler kupigwa kadi nyekundu.
Tags
Michezo