SERIKALI KUTUMIA NDEGE KUDHIBITI NZIGE LONGIDO- WAZIRI MKENDA

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda leo  ametembelea eneo la Longido ambalo yamevamiwa na nzige na kuwa kuanzia kesho ndege maalum itafanya kazi kupulizia viuatilifu kuua nzige hao.

Prof. Mkenda amesema wananchi wasiwe na hofu nzige wote watadhibitiwa kupitia wataalam wa Wizara ya Kilimo waliopo kwenye maeneo yote yenye dalili za uwepo wa wadudu hao.
"Kuanzia kesho (22.02.2021) ndege maalum itaanza kazi kupulizia sumu kuua nzige waliovamia maeneo ya Longido na Simanjiro" alisema Waziri Mkenda

Waziri Mkenda amesema tayari wataalam wa Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu vya kudhibiti visumbufu (TPRI) wapo wilayani Longido na Simanjiro wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wake Dkt. Efrem Njau .

Aidha ametoa wito kwa wananchi kutookota wala kula nzige watakaokuwa wameuawawa na viuatilifu(sumu) kwenye maeneo yote ambapo ndege itapita kuua nzige.

Pili,ameagiza wataalam na Watendaji wa vijiji na Kata kutoa taarifa Kwa wananchi juu ya uwepo wa kazi ya kuua nzige hivyo wasiwe na hofu.

"Wananchi wakiona nzige wameanguka chini wamekufa wasiwachukue au Kula kwa kuwa wengi watakuwa wamekufa Kwa sumu" alisisitiza Prof. Mkenda

Waziri huyo wa kilimo amesisitiza kuwa serikali itahakikisha mazo ya wakulima na malisho ya Mifugo hayaribiwi na nzige ndio maana ametembelea eneo hili la Longido ambapo amebainisha mafanikio ya kuwadhibiti tangu walipoingia nchini mwezi Januari mwaka huu kwenye baadhi ya maeneo.

Prof. Mkenda amesema nzige wa jangwani wana athari kubwa katika uzalishaji wa mazao ya chakula na malisho ya Mifugo na kundi moja la nzige lina uwezo wa kuruka bila kutua kwa umbali wa kilometa 150 Kwa siku.

Aidha,nzige wana uwezo wa kula Sawa na uzito wake Kwa siku ambapo kundi moja la nzige linaweza kuwa na wastani wa nzige milioni 40 kwenye eneo la kilometa moja za mraba alisema Waziri Mkenda .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Jumaa Mhina ametoa agizo shule zote za msingi na sekondari kwenye maeneo ambapo ndege itapuliza viuatilifu kusitisha masomo Kwa muda wa siku 4 kuanzia kesho ili kudhidhibi watoto wasije wakapata madhara endapo watashika au kuchezea nzige watakaokufa.

Naye Mbunge wa Longido Dkt. Steven Lemomo Kiruswa ameiomba serikali iharakishe kupulizia viuatilifu ili nzige wasije leta madhara kwa mifugo na wakulima kwenye maeneo ya Longido .

"Leo ni siku ya tatu nzige wameingia Longido, tunaomba jitihada za wataalam wa TPRI kuwadhibiti ili wasilete madhara kwetu sisi wafugaji tunaotegemea nyasi kwa malisho" alisema Mbunge Kiruswa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news