Serikali yaagiza wasiotambulika wanaouza vifaranga wa kuku wa nyama wakamatwe

Chama cha Wafugaji wa Kuku wa Nyama Tanzania (TABROFA) kimetakiwa kuwa na ushirikiano wa kutosha ili kuweza kutokomeza changamoto wanazozipata wafanyabiashara wa kuku hasa mawakala wasiotambulika wanaouza vifaranga vya kuku wa nyama pamoja na vyakula vya kuku katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akizungumza na wauzaji wa kuku wa nyama na wazalishaji wa vifaranga (hawapo pichani) baada ya kuwakutanisha na kueleza changamoto zao.Kulia ni Msajili wa Bodi ya Nyama, Bw.Imani Sichwale ambapo kikao hicho kimefanyika Februari 17, 2021 katika ofisi ndogo za wizara zilizopo Dar es Salaam.(Picha na Mwandishi Diramakini).

Akizungumza katika mkutano wa Wafanyabiashara na wazalishaji wa vifaranga vya kuku wa nyama Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ameyasema hayo jijini Dar es Salaam Februari 17, 2021 wakati akizungumza na wafanyabiashara na wazalishaji wa vifaranga wa kuku wa nyama jijini humo.

Amesema , mawakala wanaotumiwa na wenye viwanda vya kutotolesha vifaranga kama hawajasajiliwa wakamatwe ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Waziri amewataka wafugaji wote wanaouza kuku wa nyama kujisajili Bodi ya Nyama kwa ajili ya biashara kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekaidi.

Amesema, sekta ya ufugaji ni muhimu kwa pato ya nchi na kuwataka wataalamu wa mifugo kufanya tafiti za mifugo kwa kuwalenga wafugaji wenyewe kwa kubaini changamoto zao sio kuwatumia wasomi.Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Nyama, Imani Sichwale amewataka wafugaji hao kuacha kufuga kuku kwa mazoea badala yake wafuge kitaalamu kwa kuweka bajeti ya ufugaji kwa lengo la kukuza sekta yao.

Naye Mwenyekiti wa TABROFA, Bw.Costa Mrema amesema katika tafiti walizozifanya zimebaini kuwa ulaji wa kuku wa nyama Tanzania ni kati ya kuku 900,000 hadi milioni 1.2 kwa wiki huku walaji wakubwa wakiwa mkoani Dar es Salaam, Pwani, Arusha, Mwanza,Kilimanjaro na Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news