Serikali yapiga marufuku shughuli zisizo za kiuhifadhi ndani ya maeneo ya hifadhi

Serikali imepiga marufuku shughuli zote zisizo za kiuhifadhi zinazofanywa na binadamu katika maeneo yaliyohifadhiwa nchini kwa kuwa maeneo hayo ni sehemu ya mapato na vivutio nchini, anaripoti John Berra (WMU).
Marufuku hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja wakati akijibu swali la Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei bungeni jijini Dodoma mapema leo.

Amesema, Serikali imeweka maeneo ambayo ni sahihi kwa matumizi ya kibinadamu na si kufanya shughuli zisizo za kiuhifadhi ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa nchini

“Sisi kama Serikali tunapokuwa tunahifadhi haya maeneo, tunatunza ili yawe kivutio na kwa ajili ya kutuletea mapato, kwa hiyo tunapokuwa tunatunza hairuhusiwi kufanya kitu chochote ndani ya eneo la hifadhi, hataka kama ni kuokota kuni hairuhusiwi, lakini kuna maeneo mengine ambayo huwa tunawatengea wananchi kwa ajili ya kuendelea na shughuli zingine kama ufugaji, Uvuvi pamoja na Kilimo, lakini maeneo yanayotunzwa kama hifadhi hairuhusiwi kufanya Chochote,”amesema Mhe. Mary Masanja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news