TFF yaamua mechi kati ya Namungo FC na CD 1 Agosto ya Angola zichezwe nchini Tanzania

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeamua mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho kati ya CD 1 Agosto ya Angola na Namungo FC ya Tanzania zichezwe nchini Tanzania, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Uamuzi huo umefanywa baada ya Kamati ya CAF ya Mashindano hayo kubaini kuwa si Agosto wala Namungo iliyohusika moja kwa moja kukwamisha mechi ya kwanza iliyokuwa ichezwe Februari 14 nchini Angola.

Mechi zote mbili zinatakiwa kuchezwa angalau ndani ya saa 72, na ziwe zimechezwa kufikia Februari 26 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba, CD 1 Agosto itakuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza, hivyo itawajibika katika maandalizi yote ikiwemo gharama za maofisa wa mechi hiyo.

Kwa vile makundi ya Kombe la Shirikisho yatapangwa Februari 22, mshindi wa jumla baada ya mechi hizo mbili hatazingatiwa katika viwango (non-ranked) wakati wa upangaji.

No comments

Powered by Blogger.