Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today February 10th, 2021


 UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:

TAREHE: 10/02/2021.


Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe, Lindi, Mtwara Ruvuma, Dodoma, Singida, Tabora, Katavi pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, Mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.

...........

Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Shinyanga, Mara, Simiyu, Mwanza, Kagera, Geita na Kigoma: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

...........

Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga pamoja na (Visiwa vya Unguja na Pemba) na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo

machache na vipindi vya jua.

...........


ANGALIZO:

1. VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA LINDI, MTWARA, RUVUMA, NJOMBE, IRINGA, RUKWA, SONGWE, MBEYA PAMOJA NA KUSINI MWA MKOA WA MOROGORO


2. VIPINDI VYA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KM 40 KWA SAA NA MAWIMBI MAKUBWA YANAYOFIKIA MITA 2 VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA UKANDA WOTE WA PWANI KATIKA MIKOA YA LINDI, MTWARA, DAR-ES-SALAAM, TANGA NA PWANI (IKIJUMUISHA VISIWA VYA MAFIA), PAMOJA NA VISIWA

VYA UNGUJA NA PEMBA.

..........


VIWANGO VYA JOTO VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:


MJI                     Kiwango cha juu  Kiwango cha chini

                           cha joto               cha joto

ARUSHA             26°C                    18°C 

D'SALAAM          31°C                    26°C 

DODOMA           27°C                    19°C 

KIGOMA             30°C                     21°C 

MBEYA                23°C                    16°C 

IRINGA                25°C                    18°C 

NJOMBE              18°C                    11°C 

MWANZA            29°C                    21°C 

TABORA               27°C                    20°C 

TANGA                 31°C                    25°C 

ZANZIBAR            29°C                    29°C

..........

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa.

Matarajio kwa siku ya Ijumaa tarehe 12/02/2021: Mabadiliko kidogo.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 10/02/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.


Matarajio ya Hali Mbaya ya Hewa kwa siku Tano

Jumatano: Tarehe 10-02-2021


ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (pamoja na visiwa cha Mafia), Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Rukwa, Songwe, Mbeya, Dodoma, Singida na Manyara.

........

UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI 

Athari zinazoweza kujitokeza:

 Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za safirishaji.

Tafadhali zingatia na ujiandae.

..........

ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na Mawimbi makubwa yanayofikia mita 2, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.


UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

Athari zinazoweza kujitokeza: 

Kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi.

Tafadhali ZINGATIA NA UJIANDAE.

.........


Alhamisi 11- 02-2021

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Rukwa, Songwe, Mbeya pamoja na Kusini mwa mkoa wa Morogoro.


UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI


Athari zinazoweza kujitokeza:

Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji.

Tafadhali zingatia na ujiandae.

.........

ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na Mawimbi makubwa yanayofikia mita 2, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.


UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.


Athari zinazoweza kujitokeza:

Kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi.

Tafadhali ZINGATIA NA UJIANDAE.

.........

Ijumaa 12- 02-2021

ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.


UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.


Athari zinazoweza kujitokeza:

Kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi.

Tafadhali ZINGATIA NA UJIANDAE.

...........


Jumamosi 13- 02-2021 

HAKUNA TAHADHARI. 

..........


Jumapili 14- 02-2021

HAKUNA TAHADHARI.

No comments

Powered by Blogger.