TAREHE: 12/02/2021.
Mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Manyara, Kilimanjaro na Arusha: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, Mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.
.........
Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Kagera, Geita, Mara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Dodoma, Singida, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Tanga, Morogoro pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
........
ANGALIZO
VIPINDI VYA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KM 40 KWA SAA NA MAWIMBI MAKUBWA YANAYOFIKIA MITA 2 VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA UKANDA WA PWANI YA KUSINI, MIKOA YA LINDI, MTWARA, PAMOJA NA UKANDA WA ZIWA NYASA.
..........
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 24°C 16°C
D'SALAAM 30°C 25°C
DODOMA 26°C 19°C
KIGOMA 29°C 22°C
MBEYA 23°C 17°C
IRINGA 23°C 17°C
NJOMBE 17°C 11°C
MWANZA 25°C 21°C
TABORA 28°C 20°C
TANGA 30°C 24°C
ZANZIBAR 30°C 25°C
..........
Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani Ya Kaskazini; na kwa kasi ya km 40 kwa saa kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi hadi makubwa
Matarajio kwa siku ya Jumapili tarehe 14/02/2021: Mabadiliko kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 12/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.