Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today February 16th, 2021

 UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:TAREHE: 16/02/2021.

Mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Kagera, Geita, Mara, Mwanza, Kigoma, Tabora, Katavi: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........
Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma, Dodoma na Singida: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........
Mkoa wa Morogoro kwa upande wa kusini kunatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi kwa maeneo machache na vipindi vya jua.
...............
Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Tanga (Visiwa vya Unguja na Pemba) pamoja na Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
...........
Mikoa ya Lindi na Mtwara: Inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu na vipindi vifupi vya jua.
...........
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 29°C 15°C
D'SALAAM 33°C 25°C
DODOMA 30°C 20°C
KIGOMA 31°C 21°C
MBEYA 25°C 17°C
IRINGA 27°C 17°C
NJOMBE 22°C 13°C
MWANZA 30°C 20°C
TABORA 30°C 18°C
TANGA 32°C 24°C
ZANZIBAR 33°C 25°C
.............
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa.
Matarajio kwa siku ya Alhamisi tarehe 18/02/2021: Mabadiliko kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 16/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news