Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today February 19th, 2021

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:TAREHE: 19/02/2021.

 
Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Kagera, Geita, Mara, Mwanza na Rukwa: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........
Mikoa ya Shinyanga na Simiyu: Hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
........
Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe: Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
.........
Mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........
Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha: Inatarajiwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
..........
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango chachini
cha joto cha joto
ARUSHA 28°C 14°C
D'SALAAM 32°C 25°C
DODOMA 30°C 20°C
KIGOMA 30°C 21°C
MBEYA 27°C 16°C
IRINGA 28°C 17°C
NJOMBE 23°C 13°C
MWANZA 28°C 22°C
TABORA 29°C 20°C
TANGA 32°C 24°C
ZANZIBAR 32°C 24°C
..........
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo.
Matarajio kwa siku ya Jumapili tarehe 21/02/2021: Mabadiliko kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 19/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

No comments

Powered by Blogger.